Ninafikiri watu wengi tumewahi kukutana na swali, kwanini unafanyi hivi au vile? Na hata kwenye filamu moja ya marehemu Kanumba aliigiza filamu inaitwa , Why? Hilo ni swali lile lile katika mtizamo tofauti. Ukitaka kujua uwezo wa kufikiri kwako ni pale utakapojibu kwa usahihi hili swali, kwanini? Mfano; Kama wewe ni mfanyakazi ukaulizwa kwanini unafanya kazi? na kutokana na jibu lako ukaulizwa tena kwanini? na kutokana na jibu lililofuata ukaulizwa tena kwanini? na kutokana na jibu hili tena ukaulizwa kwanini? Kinachofuata hapo watu wengi huchanganyikiwa au hukasirika kwasababu huanza kuishiwa majibu au swali hilo huanza kuchimba undani na uhalisia wa mtu. Nataka niongelee umuhimu wa swali hilo katika kazi, masomo au maisha yako ya kila siku. Unapaswa kujiuliza kwanini unafanya unachokifanya, kwanini uko hapo ulipo? Kwanini unafikiri hivyo ulivyo na kwanini ni wewe? Ni eneo ambalo unaanza kuona uhalisia wa wewe na vitu unavyofanyana utagundua makosa yako mengi au mitizamo m...