TETESI ZA SOKA ULAYA
Real Madrid wamekamilisha uhamisho wa pauni milioni 20 wa Radamel Falcao, 28, kutoka Monaco (Calciomercato), Arsenal wana matumaini ya kukamilisha uhamisho wa beki Sorkatis Papastathopoulos, 26, kutoka Borussia Dortmund, lakini wamesema hawatalipa pauni milioni 20 (Daily Mirror), boss wa Aston Villa Paul Lambert ametoa dau la pauni milioni 8 kumtaka kiungo wa Manchester United Tom Cleverly, 25, (Daily Telegraph), lakini Lambert huenda wakapata upinzani mk ali kutoka Valencia, ambao nao pia wamepanda dau kwa Cleverly (Sky Sports), Danny Welbeck, 23, anajiandaa kuondoka Old Trafford, na akitajwa kwenda Tottenham kwa mkopo (Daily Star), Chelsea wanakaribia kutoa ruhusa kwa Fernando Torres, 30, kwenda A.C Milan (Times) , Manchester United wameongeza bidii kumfuatilia kiungo Martin Odegaard, 15, anayechezea Stromsgodset kutoka Norway (Daily Telegraph), Valencia na Juventus wametoa dau la kutaka kumsajili Javier Hernandez, 26, kutoka Manchester United kwa kiasi cha pauni milioni 15 (Gu...